KURUGENZI YA VIJANA (CHRIST GOSPEL MESSANGERS)

Kurungenzi ya Vijana (Christ Gospel Messangers - CGM) inahudumia vijana wa Kanisa la EAGT, wenye umri wa miaka 18 hadi 35, wa kiume na wa kike. Lengo kuu la Kurugenzi hii ni kuwaandaa na kuwanoa vijana kumtumikia Mungu, kuwa wanandoa bora wakati ukifika, kuwa wazazi mahiri Mungu atakapowajalia watoto, kuwa wanafamilia bora, na kuwajengea uwezo kujitegemea kiuchumi. Kupitia mafundisho ya Neno la Mungu, mafundisho ya stadi za kazi, ushauri na maombi, vijana wengi wamefaidika na Kurungenzi hii. Kurungenzi ya CGM pia inawajengea uwezo vijana kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi kuanzia ngazi ya familia hadi kitaasisi, ili kujiongezea kipato. Aidha, Kurugenzi ya CGM imekuwa ikiwategemeza Watumishi wa Mungu kwa namna mbalimbali, waliwemo wanaofanya huduma vijijini. Kurugenzi hii ina uongozi kuanzia ngazi ya Taifa, Kanda, Jimbo na Kanisa la mahali pamoja. Kauli mbiu ya Kurungenzi hii ni "Vijana tuna nguvu, tumejaa Neno la Mungu, na tumemshinda Shetani".

Wafuatao ni Viongozi wa Kitaifa wa Kurungenzi ya CGM wanaohudumu katika kipindi hiki:

Jina Cheo Namba ya Simu Barua-pepe ya Ofisi Barua-pepe Binafsi
Rev. Yohana Mwangupili Malakapyela Mkurugenzi - Taifa +255 755 479 308 Mkurugenzi.CGM-Taifa@eagt.or.tz Yohana.Malakapyela@eagt.or.tz
Rev. Erick Ebehart Ndunguru Makamu Mkurugenzi - Taifa +255 754 592 056 Makamu.Mkurugenzi.CGM-Taifa@eagt.or.tz Erick.Ndunguru@eagt.or.tz
Rev. Bethueli Brandani Waitara Katibu - Taifa +255 683 149 129 Katibu.CGM-Taifa@eagt.or.tz Bethueli.Waitara@eagt.or.tz
Rev. Paulo Thomas Nyabagaka Mhazina - Taifa +255 754 436 797 Mhazina.CGM-Taifa@eagt.or.tz Paulo.Nyabagaka@eagt.or.tz