KURUGENZI YA VIJANA WA SEKONDARI NA VYUO (CHRIST GOSPEL MESSANGERS STUDENTS' FELLOWSHIP)

Kurungenzi ya Vijana wa Sekondari na Vyuo (Christ Gospel Messangers Students' Fellowship - CGMSF) inahudumia vijana wa Kanisa la EAGT, walio katika shule za sekondari (elimu ya upili), vyuo vya ufundi na mafunzo ya amali, na vyuo vikuu. Lengo kuu la Kurugenzi hii ni kuwaandaa na kuwanoa vijana hawa kuilinda imani wawapo masomoni, kufanya vizuri katika masomo yao na kufaulu kwa viwango vya juu, kumtumikia Mungu, kuwa wanandoa bora wakati ukifika, kuwa wazazi mahiri Mungu atakapowajalia watoto, kuwa wanafamilia bora, na kuwajengea uwezo kujitegemea kiuchumi. Kurugenzi hii pia ina lengo la kuhubiri injili mashuleni na vyuoni ili kuwavuta wanafunzi wengi kwa Yesu, tukiamini kwamba vijana hawa wakimpata Yesu katika umri mdogo, wataepushwa na uharibifu wa Shetani na kuwa nguvu-kazi yenye tija kwa Taifa na Ufalme wa Mungu. Kupitia mafundisho ya Neno la Mungu, mafundisho ya stadi za kazi, ushauri na maombi, vijana wengi wa shule za sekondari na vyuoni wamefaidika na Kurungenzi hii. Kurugenzi hii ina uongozi kuanzia ngazi ya Taifa, Kanda na Jimbo.

Wafuatao ni Viongozi wa Kitaifa wa Kurungenzi ya CGMSF wanaohudumu katika kipindi hiki:

Jina Cheo Namba ya Simu Barua-pepe ya Ofisi Barua-pepe Binafsi
Rev. Ayubu Kitangita Birahi Mkurugenzi - Taifa +255 763 709 671 Mkurugenzi.CGMSF-Taifa@eagt.or.tz Ayubu.Kitangita@eagt.or.tz
Rev. Suleiman Peter Madaha Makamu Mkurugenzi - Taifa +255 752 571 838 Makamu.Mkurugenzi.CGMSF-Taifa@eagt.or.tz Suleiman.Madaha@eagt.or.tz
Rev. Agustino William Mkalawa Katibu - Taifa +255 620 693 132 Katibu.CGMSF-Taifa@eagt.or.tz Agustino.Mkalawa@eagt.or.tz
Rev. Wambura Anthony Sanga Mhazina - Taifa +255 617 133 811 Mhazina.CGMSF-Taifa@eagt.or.tz Wambura.Sanga@eagt.or.tz