IMANI YA EAGT
EAGT ina Imani moja ya Mungu Mmoja nafsi tatu; Biblia moja; Katiba moja na Dira moja. Katika Dira ya EAGT ya mwaka 2020 hadi 2034, maono yetu ni “Habari njema ya wokovu kuwafikia watu wote nchini Tanzania na nje ya nchi” (Warumi 1:16-17). Tuna Maadili ya msingi saba yanayogusia; ibada; zaka na sadaka; sifa na kuabudu; kufunga na kuomba; Neno la Mungu; kuwaleta watu kwa Yesu na shukrani kwa Mungu. Tuna nguzo tatu ambazo ni Utakatifu, Uongozi, na Utoaji; ambazo zimebeba Vipaumbele saba vinavyohusiana na kuhubiri Injili, kuimarisha Uongozi, elimu ya Teolojia, huduma za jamii, kumiliki ardhi, ujenzi wa ofisi za utawala, na kumiliki mawasiliano.