The Evangelistic Assemblies of God(T)
EAGT ina imani moja ya Mungu Mmoja nafsi tatu; biblia moja,katiba moja na sasa dira moja! .
"HABARI NJEMA IMEWAFIKIA WATU WOTE"
Dira Yetu
Habari Njema Imewafikia Watu Wote.
Dhima
Kuwa Kanisa moja lenye nguvu za kiroho za kutenda, kumiliki na kuwafikia maelfu ya watu kwa Neno la Mungu, tukiwafundisha kuyashika yote aliyosema Yesu Kristo ili kuwa na Jamii imara iliyofanikiwa kiroho, kiafya, kifikra, kiuchumi, na mambo yote na hatimaye wateule wapate Uzima wa Milele.
Kauli Mbiu
Habari njema kwa wote.
![]() |
"Tunarudisha utukufu wote, heshima na shukrani kwa Mungu kwa kutujalia mavuno haya. Tangu Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) ilipoanza huduma yake katika taifa hili, chini ya uongozi wa hayati Mch. Dkt. Moses Samuel Kulola, uongozi wa Kanisa umeendelea kuimarishwa kuanzia ngazi ya kitaifa hadi Kanisa la Mahali Pamoja. Katika kuimarisha na kuboresha huduma yake, EAGT inaendelea kusimama imara katika kushikilia Neno la Mungu na inaongozwa na katiba iliyoasisiwa juu ya Tamko la Imani la dhehebu na misingi yake mikuu ya mafundisho." Dkt. Brown Abel Mwakipesile(Askofu Mkuu) |
Kuhusu Kanisa
Shule na Vyuo Vyetu
Kanisa la EAGT lina vyuo vya theolojia katika nchi nzima pamoja na Shule ya sekondari
Umuhimu wa elimu
Kwa kutambua umuhimu wa Elimu kama kama maandiko yasemavyo; Kanisa limeweka juhudi mahsusi ya kuwekeza katika elimu na ufundi.Shule zinazomilikiwa na Kanisa zinalenga kutoa elimu bora ya kitaaluma ikiambatana na maadili ya Kikristo na malezi ya kiroho kwa wanafunzi. Pichani ni shule ya kwanza ya Sekondari ya OASIS inayomilikiwa na kanisa. Shule hii ambayo ina vidato vinne ipo katika Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga.
Miradi iliyoanzishwa na Idara ya MIMA
(Mipango, Miradi na Maendeleo)
Kuenea kwa Kanisa
Kanisa la EAGT limeenea katika mikoa yote na wilaya zote nchini Tanzania, pamoja na nchi mbalimbali za jirani ikiwemo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC), Kenya, Malawi, Msumbiji, Rwanda na Zambia. Ashukuriwe Mungu anayewawezesha watumishi wake kufanya kazi ya kuhubiri Injili hata nje ya mipaka ya Tanzania.
Church is a refuge from the chaos of everyday life—a place where you can worship God with other believers trying to be more like Jesus. We would love to have you believe in Jesus Christ and get saved!
Kanisa pia huendesha Bible Colleges (Vyuo vya Biblia) ambavyo hutoa mafunzo ya theolojia kwa wachungaji na viongozi.
Shule za Kanisa-EAGT
