DONDOO ZA MPANGO MKAKATI

MAONO YETU: Habari njema ya wokovu kuwafikia watu wote nchini Tanzania na nje ya nchi (Warumi 1:16, Isaya 55:11; Luke 4:18-19, Habakuki 2:2-3).

DHIMA YETU: Kuwa Kanisa moja (Waefeso 4:4- 7) lenye nguvu za kiroho za kutenda, kumiliki na kuwafikia maelfu ya watu kwa Neno la Mungu, tukiwafundisha kuyashika yote aliyosema Yesu Kristo ili kuwa na Jamii imara iliyofanikiwa kiroho, kiafya, kifikra (Joshua 1:8, Zaburi 119:15, Wafillipi 4:8, Malaki 3:16), kiuchumi, na mambo yote (3Yohana 3) na hatimaye wateule wapate Uzima wa Milele; (Wakolosai 1:28; Yohana 12:26; Luka 4:21-22; 1Wakorintho 4:1-2).

NGUZO ZETU TATU: Utakatifu, Uongozi na Utoaji
 
MAADILI SABA YA MSINGI: i. Ibada ii.Zaka na Sadaka iii. Sifa na Kuabudu vi. Neno la Mungu v. Kufunga na Kuomba vi. Kushuhudua Injili vii. Shukrani
 
MALENGO YETU 12
Lengo la 1: Kuihubiri Injili iliyo hai ya kuwafanya watu wawe wanafunzi wa Yesu ili Kanisa liongezeke na watu waokolewe. (Marko 16:20; Matendo ya Mitume 26:16-18).
Lengo la 2: Kuwafanya waliompokea Yesu kuwa wanafunzi wa Yesu na kuwafundisha kushika yote (Mathayo 28:20, Wakolosai 3:16).
Lengo la 3: Kujenga na kuimarisha uwezo wa viongozi ngazi zote kufanya maamuzi kwa kutumia takwimu na kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
Lengo la 4: Kuboresha elimu ya Teolojia ili kila Mchungaji awe na stashahada na Shahada ya kwanza ifikapo 2034.Lengo la 4 Kuboresha elimu ya Teolojia ili kila Mchungaji awe na stashahada na Shahada ya kwanza ifikapo 2034.
Lengo la 5: Kuanzisha miradi mbali mbali ya Huduma za Jamii ikiwemo; elimu, afya na maji.
Lengo la 6: Kuboresha hali za maisha ya washirika Kanisani kupitia Huduma za Jamii.
Lengo la 7: Kuboresha mazingira ya utendaji na utawala wa Kanisa la EAGT Shughuli muhimu za kufikia malengo.
Lengo la 8: Ifikapo mwaka 2022 Makanisa mengi yawe yanamiliki maeneo makubwa ya Kanisa kwa ajili ya maendeleo na Huduma za Jamii.
Lengo la 9: Kumiliki vyombo vya habari ili kuwafikia watanzania wengi kwa neno la Mungu kwa urahisi zaidi.
Lengo la 10: Kuimarisha mshikamano na uwezo wa pamoja wa EAGT kifedha kwa ajili ya kufanikisha vipaumbele vya Kitaifa ifikapo mwaka 2021.
Lengo la 11: Kutumia raslimali zitokanazo na hazina ya taifa kwa weledi na uaminifu sawasawa na mipango maalum iliyokubalika kuanzia Januari 2020 (Mathayo 25:21).
Lengo la 12: Kuandaa na kuboresha mfumo wa taarifa na ufuatiliaji wa EAGT ifikapo 2020.

 

Kusoma zaidi kuhusu Mpango Mkakati wa EAGT Bonyeza hapa ....