VIONGOZI WAKUU WA KANISA LA EAGT
Askofu. Dkt. Brown Abel MwakipesileAskofu. Dkt. Brown Abel Mwakipesile ni Askofu Mkuu wa pili wa Kanisa la EAGT. Alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu kwa mara ya kwanza mwezi Septemba 2015. Kwa neema ya Mungu na kwa imani kubwa ambayo Mkutano Mkuu wa Kanisa la EAGT uliionesha kwake, alichaguliwa tena kuwa Askofu Mkuu mwezi Septemba 2020 na Septemba 2025. Kabla ya kuchaguliwa kuwa Askofu Mkuu, Askofu Mwakipesile alikuwa Katibu Mkuu wa Kanisa la EAGT tangu mwaka 1993, wakati Askofu Mkuu akiwa Hayati Dkt. Moses Samwel Kulola. |
![]() |
Askofu Dkt. Joshua Benjamini WawaAskofu Dkt. Joshua Benjamini Wawa ni Makamu Askofu Mkuu wa nne wa Kanisa la EAGT. Alichaguliwa kuwa Makamu Askofu Mkuu kwa mara ya kwanza mwezi Septemba 2020. Kwa neema ya Mungu na kwa imani kubwa ambayo Mkutano Mkuu wa Kanisa la EAGT uliionesha kwake, alichaguliwa tena kuwa Makamu Askofu Mkuu mwezi Septemba 2025. Kabla ya kuwa Makamu Askofu Mkuu, Askofu Wawa alishika nafasi mbalimbali za uongozi katika Kanisa la EAGT, ikiwemo nafasi ya Mhazina Mkuu wa EAGT tangu mwaka 2002 hadi 2015. Watangulizi wake kwenye nafasi ya Makamu Askofu Mkuu ni Askofu Moses Mwamwenda, Askofu Asumwisye Mwaisabila na Askofu John Mahene. |
![]() |
Askofu Dkt. Leonard Majura MwizarubiAskofu Dkt. Leonard Majura Mwizarubi ni Katibu Mkuu wa tatu wa Kanisa la EAGT. Alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu kwa mara ya kwanza mwezi Septemba 2015. Kwa neema ya Mungu na kwa imani kubwa ambayo Mkutano Mkuu wa Kanisa la EAGT uliionesha kwake, alichaguliwa tena kuwa Katibu Mkuu mwezi Septemba 2020 na Septemba 2025. Kabla ya kuwa Katibu Mkuu, Askofu Mwizarubi alikuwa Askofu wa Kanda ya Kaskazini tangu mwaka 1993. Watangulizi wake kwenye nafasi ya Katibu Mkuu ni Askofu Mark Mhina na Askofu Brown Abel Mwakipesile. |
![]() |
Askofu Dkt. PrayGod Zawadi MgonjaAskofu Dkt. PrayGod Zawadi Mgonja ni Mhazina Mkuu wa nne wa Kanisa la EAGT. Alichaguliwa kuwa Mhazina Mkuu kwa mara ya kwanza mwezi Septemba 2015. Kwa neema ya Mungu na kwa imani kubwa ambayo Mkutano Mkuu wa Kanisa la EAGT uliionesha kwake, alichaguliwa tena kuwa Mhazina Mkuu mwezi Septemba 2020 na Septemba 2025. Kabla ya kuwa Mhazina Mkuu, Askofu Mgonja alishika nafasi mbalimbali za uongozi katika Kanisa la EAGT, ikiwemo nafasi Katibu wa jimbo la Kinondoni na Mhazina wa Kanda ya Mashariki. Watangulizi wake kwenye nafasi ya Mhazina Mkuu ni Askofu Mark Mhina, Askofu Erastus Andrew na Askofu Joshua Wawa. |
|
Askofu Dkt. Livingstone Denes ManiyanguruAskofu Dkt. Livingstone Denes Maniyanguru ni Mshauri Mkuu wa pili wa Kanisa la EAGT. Alichaguliwa kuwa Mshauri Mkuu kwa mara ya kwanza mweziSeptemba 2020. Kwa neema ya Mungu na kwa imani kubwa ambayo Mkutano Mkuu wa Kanisa la EAGT uliionesha kwake, alichaguliwa tena kuwa Mshauri Mkuu mwezi Septemba 2025. Kabla ya kuwa Mshauri Mkuu, Askofu Denes alishika nafasi mbalimbali za uongozi katika Kanisa la EAGT ikiwemo nafasi ya Askofu wa Kanda ya Kati tangu mwaka 2005. Mtangulizi wake kwenye nafasi ya Mshauri Mkuu ni Askofu Anyandwile Mwakisyala. |
![]() |



