KURUGENZI YA UINJILISTI (THE EAGT BOARD OF EVANGELISM)

Kurungenzi ya Uinjilisti (The Evangelistic Board of Evangelism - TEBE) ina jukumu la kuratibu huduma ya uinjilisti katika Kanisa la EAGT. Lengo kuu la Kurugenzi hii ni kuwaandaa na kuwanoa Wainjilisti ili wawashe moto wa injili na kuwavuta watu wengi kwa Yesu, ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Kurugenzi hii inasimamia utekelezaji wa Agizo Kuu la Bwana Yesu (The Great Commission), ambalo ni "Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Kurugenzi hii, na Kanisa la EAGT kwa ujumla linaamini kwamba, Injili ya kweli ni suluhisho namba moja la matatizo yote ya kiroho, kimwili, kijamii na kimaendeleo kwa watu. Jamii yoyote ikimjua Mungu vizuri na kuishi maisha yenye maadili mema, lazima itapata maendeleo endelevu. Kurugenzi ya TEBE ina uongozi kuanzia ngazi ya Taifa, Kanda na Jimbo.

Wafuatao ni Viongozi wa Kitaifa wa Kurungenzi ya TEBE wanaohudumu katika kipindi hiki:

Jina Cheo Namba ya Simu Barua-pepe ya Ofisi Barua-pepe Binafsi
Mwj. Emmanuel Kasalwika Mwaijala Mkurugenzi - Taifa +255 755 775 434 Mkurugenzi.TEBE-Taifa@eagt.or.tz Emmanuel.Mwaijala@eagt.or.tz
Mwj. Simon Paulo Gwamwanza Makamu Mkurugenzi - Taifa +255 754 447 966 Makamu.Mkurugenzi.TEBE-Taifa@eagt.or.tz Simon.Gwamwanza@eagt.or.tz
Mwj. Andulile Asajile Mbwile Katibu - Taifa +255 767 755 619 Katibu.TEBE-Taifa@eagt.or.tz Andulile.Mbwile@eagt.or.tz
Mwj. Thadei Paul Kamonga Mhazina - Taifa +255 754 773 086 Mhazina.TEBE-Taifa@eagt.or.tz Thadei.Kamonga@eagt.or.tz