KURUGENZI YA WANAUME WA HUDUMA YA INJILI
Kurungenzi ya Wanaume Huduma ya Injili (WHI) inahudumia wanaume wa Kanisa la EAGT, ikijumuisha wanaume walio kwenye ndoa, wanaume au vijana ambao wanajiandaa kuingia kwenye ndoa na wagane. Lengo kuu la Kurugenzi hii ni kuwaandaa na kuwanoa wanaume kumtumikia Mungu, kuwa nguzo imara na viongozi wa familia, na kuwajengea uwezo kujitegemea kiuchumi. Kupitia mafundisho ya Neno la Mungu, mafundisho ya stadi za kazi, ushauri na maombi, wanaume wengi wamefaidika na Kurungenzi hii. Kurungenzi ya WHI pia inawajengea uwezo wanaume kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi kuanzia ngazi ya familia hadi kitaasisi, ili kujiongezea kipato. Aidha, Kurugenzi ya WHI imekuwa ikiwategemeza Watumishi wa Mungu kwa namna mbalimbali, waliwemo wanaofanya huduma vijijini. Kurugenzi hii ina uongozi kuanzia ngazi ya Taifa, Kanda, Jimbo na Kanisa la mahali pamoja. Kauli mbiu ya Kurungenzi hii ni "Mwanaume ni Nguzo na Kiongozi".
Wafuatao ni Viongozi wa Kitaifa wa Kurungenzi ya WHI wanaohudumu katika kipindi hiki:
(Mkurugenzi - Taifa)
(Makamu Mkurugenzi - Taifa)
(Katibu - Taifa)
(Mhazina - Taifa)
| Jina | Cheo | Namba ya Simu | Barua-pepe ya Ofisi | Barua-pepe Binafsi |
|---|---|---|---|---|
| Rev. Madaraka Ndenjela Sindondwa | Mkurugenzi - Taifa | +255 755 813 394 | Mkurugenzi.WHI-Taifa@eagt.or.tz | Madaraka.Sindondwa@eagt.or.tz |
| Rev. Simon Joseph Masele | Makamu Mkurugenzi - Taifa | +255 678 820 444 | Makamu.Mkurugenzi.WHI-Taifa@eagt.or.tz | Simon.Masele@eagt.or.tz |
| Rev. Mathew Francis Mbalinga | Katibu - Taifa | +255 784 394 964 | Katibu.WHI-Taifa@eagt.or.tz | Mathew.Mbalinga@eagt.or.tz |
| Rev. Jocktan Samwel Mohamed | Mhazina - Taifa | +255 755 778 696 | Mhazina.WHI-Taifa@eagt.or.tz | Jocktan.Mohamed@eagt.or.tz |