KURUGENZI YA WANAWAKE WA INJILI
Kurungenzi ya Wanawake wa Injili (WWI) inahudumia wanawake wa Kanisa la EAGT, ikijumuisha wanawake walio kwenye ndoa, wanawake au mabinti ambao wanajiandaa kuingia kwenye ndoa na wajane. Lengo kuu la Kurugenzi hii ni kuwaandaa na kuwanoa wanawake kumtumikia Mungu, kuwa msingi imara wa familia, na kuwajengea uwezo kujitegemea kiuchumi. Kupitia mafundisho ya Neno la Mungu, mafundisho ya stadi za kazi, ushauri na maombi, wanawake wengi wamefaidika na Kurungenzi hii. Kurungenzi ya WWI pia inatekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi, inayoiwezesha kuingiza kipato. Aidha, Kurungenzi ya WWI imekuwa ikiwategemeza Watumishi wa Mungu kwa namna mbalimbali, wakiwemo wanaofanya huduma vijijini. Kurugenzi hii ina uongozi kuanzia ngazi ya Taifa, Kanda, Jimbo na Kanisa la mahali pamoja. Kauli mbiu ya Kurungenzi hii ni "Wanawake wa Injili ni Jeshi Kubwa".
Wafuatao ni Viongozi wa Kitaifa wa Kurungenzi ya WWI wanaohudumu katika kipindi hiki:
(Mkurugenzi - Taifa)
(Makamu Mkurugenzi - Taifa)
(Katibu - Taifa)
(Mhazina - Taifa)
| Jina | Cheo | Namba ya Simu | Barua-pepe ya Ofisi | Barua-pepe Binafsi |
|---|---|---|---|---|
| Mrs. Beatrice PrayGod Mgonja | Mkurugenzi - Taifa | +255 754 369 145 | Mkurugenzi.WWI-Taifa@eagt.or.tz | Beatrice.Mgonja@eagt.or.tz |
| Mrs. Leah John Mafwimbo | Makamu Mkurugenzi - Taifa | +255 754 472 205 | Makamu.Mkurugenzi.WWI-Taifa@eagt.or.tz | Leah.Mafwimbo@eagt.or.tz |
| Mrs. Amesario Leonard Mwizarubi | Katibu - Taifa | +255 754 461 402 | Katibu.WWI-Taifa@eagt.or.tz | Amesario.Mwizarubi@eagt.or.tz |
| Mrs. Specioza Anthony Jokakuu | Mhazina - Taifa | +255 767 820 717 | Mhazina.WWI-Taifa@eagt.or.tz | Specioza.Jokakuu@eagt.or.tz |